Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, tarehe 29 Aprili 2025, inayosadifiana na siku ya kwanza ya Mwezi wa Dhul-Qa'dah katika kalenda ya Hijria, kituo cha Kiislamu cha Madrasat Al-Hadi (as) kilichopo chini ya Usimamizi na Uwakilishi wa Al-Mustafa (s) nchini Malawi, kimeandaa hafla maalum ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Bibi Mtukufu, Fatima Maasumah (s.a).
Kituo cha Kiislamu cha Madrasat Al-Hadi (as) kilichopo chini ya Usimamizi na Uwakilishi wa Al-Mustafa (s) nchini Malawi, kimefanikiwa kuandaa hafla maalum ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Bibi Mtukufu, Hazrat Fatima Maasumah (s.a).
Sherehe hii iliambatana na mihadhara ya kielimu, qaswida, dua, na nasaha kuhusu nafasi ya Mwanamke katika Uislamu kulingana na mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s). Washiriki walipata fursa ya kutafakari maisha ya Bibi Fatima Maasumah (s.a), ambaye alikuwa ni kielelezo cha Elimu, Ucha Mungu, na Heshima kwa Wanawake wa Kiislamu.
Al-Mustafa International Foundation, ikiongozwa na Hojjat al-Islam wal-Muslimin Dr.Ali Taqavi, inaendelea kuhuisha maadhimisho ya tukio hili muhimu kama njia ya kukuza maarifa ya Kiislamu, umoja wa waumini, na kuenzi urithi wa Ahlul Bayt (a.s) katika jamii ya Malawi.
Your Comment